Tetesi za soka Ulaya Jumatatu: Gyokeres kutua Arsenal, Chelsea wataka £50mil kwa Madueke
Chelsea wanatarajia kupokea ofa ya zaidi ya pauni milioni 50 kwa ajili ya mshambuliaji wao wa England mwenye umri wa miaka 23, Noni Madueke, ambaye amekubaliana masharti binafsi na Arsenal kuhusu uhamisho. (Telegraph)
Mshambuliaji wa Sporting mwenye umri wa miaka 27 kutoka Sweden, Viktor Gyokeres, yuko tayari kutoa takriban pauni milioni 2 za mshahara wake ili kusaidia uhamisho wake wa pauni milioni 70 kwenda Arsenal. (Record)
Tottenham na West Ham bado wako kwenye mazungumzo kuhusu uhamisho wa kiungo wa Ghana, Mohammed Kudus, baada ya West Ham kukataa ofa ya awali ya pauni milioni 50 kwa ajili ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24. (Sky Sports)
Borussia Dortmund wanataka kuongeza mkataba wa mkopo wa kiungo wa Chelsea, Carney Chukwuemeka, mwenye umri wa miaka 21, huku kipengele cha kumtoa kwa pauni milioni 40 mchezaji huyo kinda wa England kikifanya uhamisho wa kudumu kuwa mgumu. (Talksport)
CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES
Mshambuliaji wa Nigeria, Victor Osimhen, yuko tayari kujiunga na Galatasaray, ambako alikuwa kwa mkopo msimu uliopita, lakini klabu hiyo ya Uturuki italazimika kuilipa Napoli pauni milioni 65 ili kumsajili, kwani klabu hiyo ya Italia haiko tayari kumtoa chini ya hapo. (Corriere dello Sport).
Crystal Palace wako karibu kukamilisha usajili wa beki wa kushoto wa Ajax mwenye umri wa miaka 27, Borna Sosa, kwa pauni milioni 2. (Athletic)
Mshambuliaji wa Koln, Damion Downs, anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya Southampton Jumanne. Mmarekani huyo mwenye umri wa miaka 21 atasaini mkataba wa miaka minne na klabu hiyo ya Championship. (Florian Plettenberg)
Roma wanavutiwa na kumsajili kiungo wa Brighton na Denmark mwenye umri wa miaka 24, Matt O’Riley. (La Gazetta Dello Sport)
Leeds wanavutiwa na Anton Stach wa Hoffenheim lakini huenda watakabiliwa na ushindani wa kumsajili kiungo huyo wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 26. (Kicker)
CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES
Kiungo wa Everton mwenye umri wa miaka 35 kutoka Senegal, Idrissa Gueye, amesaini mkataba mpya utakaodumu hadi 2027. (Fabrizio Romano)
Mkurugenzi wa michezo wa Genoa, Flavio Ricciardella, alikubaliana na mkataba wa kumsajili Jamie Vardy, lakini meneja Patrick Vieira alikataa uhamisho wa mshambuliaji huyo wa zamani wa England mwenye umri wa miaka 38, ambaye aliachwa na Leicester wiki iliyopita. (La Repubblica)
Norwich wamekubali mkataba wa kumsajili beki wa Denmark mwenye umri wa miaka 23, Mathias Kvistgaarden, kutoka Brondby. (Tipsbladet)