Tetesi za soka Jumapili: Zubimendi akubali kujiunga na Arsenal

Tetesi za soka Jumapili: Zubimendi akubali kujiunga na Arsenal

Kiungo wa kati wa Real Sociedad Martin Zubimendi, 26, amekubali kwa mdomo kujiunga na Arsenal na mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania ananuia kujiunga na The Gunners wakati kipengele chake cha kuachiliwa cha euro 60m (£50.75m) kitakapoanzishwa. (Sportsport)

Hata hivyo, ripoti kutoka Uhispania zinasema Xabi Alonso amemjumuisha Zubimendi kwenye orodha ya walengwa wa uhamisho wa wakati, kama inavyotarajiwa, meneja wa Bayer Leverkusen atachukua nafasi ya Carlo Ancelotti kama kocha wa Real Madrid. (AS)

Klabu ya Saudi Pro League Al-Hilal inapanga kukutana kwa mara ya tatu na wawakilishi wa mchezaji wa kimataifa wa Ureno Bruno Fernandes huku wakijaribu kumshawishi mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 ajiunge nao, licha ya meneja wa Manchester United Ruben Amorim kusema anataka kiungo huyo abaki Old Trafford. (Mirror)

  Bruno Fernandes

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES

Kocha wa zamani wa Manchester United Erik ten Hag na mkufunzi wa Como Cesc Fabregas ndio wanaowania kuchukua mikoba ya Xabi Alonso katika klabu ya Bayer Leverkusen. (Kicker)

Mkurugenzi wa michezo wa Arsenal Andrea Berta anafanyia kazi mpango wa kuleta mshambuliaji mpya, na hivyo kupunguza mawindo kwa nyota wa Sporting wa Uswidi Viktor Gyokeres, 26, na mchezaji wa kimataifa wa Slovenia wa RB Leipzig Benjamin Sesko, 21. (TBR Football)

Mshambuliaji wa Ubelgiji Leandro Trossard pia yuko kwenye mazungumzo na Arsenal kuhusu mkataba mpya, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 akivutiwa na vilabu vya Saudi Pro League. (Mail)

Leandro Trossard

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES

Mustakabali wa mshambuliaji wa Ureno Cristiano Ronaldo katika klabu ya Al-Nassr uko shakani, huku mkataba wa nyongeza wa miaka miwili wa mchezaji huyo wa miaka 40 ukisitishwa. (Marca)

Manchester United wanapendelea uhamisho wa winga wa Bournemouth na Ghana Antoine Semenyo, 25, juu ya uwezekano wa kumnunua mshambuliaji wa Brentford kutoka Cameroon Bryan Mbeumo, 25. Pia wanatafuta kumsajili mshambuliaji wa Wolves wa Brazil Matheus Cunha, 25, na kiungo wa mbele wa Ipswich Town, 22, Muingereza Liam Delap. (Sky Sports viaTeamtalk)

Winga wa Ujerumani Leroy Sane hajaridhishwa na mkataba mpya unaotolewa na Bayern Munich na huenda akaondoka bila malipo msimu wa joto, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 akihusishwa na Arsenal, Chelsea au La Liga. (Sky Sport Germany)

Leroy Sane

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES

Mlinzi wa kati wa Bayer Leverkusen Jonathan Tah, 29, amehusishwa na Bayern Munich na Barcelona kwa uhamisho wa bila malipo msimu wa joto na mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani anasema atafanya uamuzi hivi karibuni kuhusu mustakabali wake. (Sport Bild)

Marseille wanamfikiria mlinzi wa kati wa Arsenal na Poland Jakub Kiwior mwenye umri wa miaka 25 kama moja ya chaguo la kuimarisha safu yao ya ulinzi msimu wa joto. (Foot Mercato – in French)

Ufitinema Aime Gerard

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *