Je, Man United kumtimua kocha wake?

Je, Man United kumtimua kocha wake?

Wiki kadhaa hadi saa za mwisho kabla ya Manchester United kukutana na Tottenham katika fainali ya Europa Ligi, ujumbe ndani ya Old Trafford ulikuwa wazi: Tufungwe au tushinde klabu itasalia na Ruben Amorim.

Wakati huo walikuwa na matumaini kwamba hawatalazimika kuuweka hadharani msimamo huo.

Lakini hicho ndicho alichofanya Amorim mwishoni mwa mkutano wake na waandishi wa habari baada ya kushindwa 1-0 mjini Bilbao.

Amorim alikuwa ameanza tathmini yake baada ya mechi kwa kauli rahisi: “Sitazungumzia hatima ya siku zijazo.”

Lakini aliishia kufanya hivyo alipoombwa kuwafariji mashabiki wa klabu hiyo baada ya msimu huo mbaya.

“Sina cha kuwaambia mashabiki,” alisema. “Kwa hiyo katika nyakati kinachohitajika ni imani hata kama ni kidogo.

“Wacha tuone hali itakavyokuwa. Niko tayari kwa lolote. Ikiwa viongozi na mashabiki wanahisi sifai, nitaondoka bila ya kuwa na kinyongo ama kuzungumzia fidia.

“Lakini sitaondoka. Ninajiamini sana linapokuja suala la utendaji wangu. Na kama unavyoona, sitabadilisha chochote katika jinsi ninavyofanya mambo.”

Afisa mkuu Omar Berrada alinishinikiza kuondoka Sporting msimu uliopita kwa sababu alihisi United ingekuwa na nafasi ya kufanya vyema ikiwa kocha atapata nafasi ya kunoa vizuri kikosi chake ipasavyo.

Amorim

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES

Maoni ya awali kutoka kwa wenye ushawishi mkubwa katika uga wa Old Trafford waliposikia alichosema Amorim iliashiria kitu kimoja – msimamo uliofikiwa wakati wa maandalizi ya mechi hiyo ya fainali kuhusu kumuunga mkono Amorim bado haujabadilika.

Na imani ya wakuu wa klabu hiyo ni kwamba wanaungana na mashabiki ambao wanatarajia kumshangilia Amorim kwa nguvu zaidi siku ya Jumapili watakapokabiliana na Aston Villa ambao, bado wana matumaini ya kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao.

Amorim alisema United walikuwa na ”mipango miwili” wanapoelekea katika soko la uhamisho wa wachezaji msimu huu wa kiangazi.

Kwa mara ya pili tangu klabu hiyo ya Uingereza iliporejea katika michuano ya Ulaya mwaka1990, haitakuwa ikijiandaa kwa michuano yoyite ya Ulaya, wala kuwa na ushawishi wa kuvutia wachezaji wa ngazi ya juu kujiunga nao.

Ikiwa Sir Jim Ratcliffe ataendelea na mpago wa kubana matumizi , basi matumizi ya fedha yatafuatiliwa kwa makini zaidi.

Nia ya mshambuliaji wa Wolves Matheus Cunha bado ingalipo. Angalau angeleta historia ya kufunga mabao kwenye Ligi kuu England

Ni Bruno Fernandes pekee katika kikosi cha sasa aliye na sifa ya ufungaji mabao. Hii inamaanisha kuwa kipaumbele cha klabu hiyo sasa ni kumsajili mshambuliaji baada ya kichapo cha Bilbao. Kwa mara ya 15 msimu huu, au mara ya 11 katika mechi 33 zilizopita, au mara ya tatu mfululizo – United walishindwa kutikisa nyavu.

“Ilionekana wazi tulikuwa timu bora, basi tu hatukufanikiwa kufunga bao kwa mara nyingine tena,” alisema Amorim.

“Kuna baadhi ya matukio msimu huu ambapo hatukuwa na mbinu za kusuluhisha hali hiyo. Lakini hili halikuwa mojawapo.

“Sio la mtu mmoja. Ni wachezaji tofauti.”

Afukuzwe au asalie?

Wiki iliyopita, wakati Amorim alisema “tunapaswa kuwa na ujasiri,” alimaanisha hilo kwa klabu nzima.

Lakini ni mambo gani hasa anayogusia?

Rasmus Hojlund ametajwa kama “mchezaji wa daraja la chini la Championship” na mtu aliyekuwa sehemu ya vyumba vya kubadilishia nguo wakati wa siku za mwisho za Sir Alex Ferguson. Inaonekana ni ukosoaji mkali. Lakini ndiyo ukweli.

Mason Mount alizungumza kwa ustadi kabla ya mechi hii lakini hakuonekana kabisa uwanjani Kaskazini mwa Hispania. Amad Diallo alionyesha kidogo uwezo lakini matokeo yake hayakuwa na tija.

Ikionekana kama bahati kubwa kwa bao la ushindi la Tottenham. Lakini mara baada ya bao hilo, Sours hawakuonekana kuwa kwenye hatari ya kupoteza.

“Mie ni mkweli daima,” alisema Amorim. “Usiku wa leo, tunahitaji kukabiliana na maumivu ya kupoteza mechi hii.”

Lakini jukumu lake la kwanza ni kukabiliana na Aston Villa siku ya Jumapili timu ambayo inawania kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uajo.

Baada ya hapo, aongoze mechi mbili barani Asia ili kuingiza mapato ya takriban pauni milioni 10, ambazo haziwahusu sana wachezaji wa United.

Makundi ya mashabiki yalitishia kufanya maandamano kwenye mechi dhidi ya Villa hata kabla ya kipigo hiki cha Spurs kwenye Europa Ligi.

Amorim lazima awafanya wachezaji wake kuonyesha mshikamano kwa njia zote kwa macho na kihisia.

Ilikuwa dhahiri kwamba Tottenham walipokuwa wakisherehekea ushindi wao, wachezaji wa United, karibu kila mmoja, alikuwa peke peke yake wakijawa na mawazo.

Andre Onana alikaa kwenye eneo lake la penati, Harry Maguire alikuwa mbele zaidi kwenye dimba hilo, Alejandro Garnacho alikua karibu na mstari wa katikati.

Amorim alikuwa akitembea huku na huko, kama kawaida yake, akitazama chini.

Hali hii ya wachezaji wanaoonuesha kuumia na kuvunjika na imani, Amorim lazima aunde kikosi chenye uwezo wa kuiwakilisha vilivyo klabu hii yenye historia kubwa kws misimu ijayo kama atasalia.

Atabebwa hadi lini?

Mshikamano unaonekana bado upo,na lengo la kumbakisha linaonekana lakini kwa muda gani?

Kwa takwimu Amorim ameshinda mechi sita pekee kwenye Ligi kuu msimu huu, nusu yake dhidi ya timu zilizoshuka daraja.

Kuna dalili za kurejea kwa yaliyotokea msimu wa 2021-2022 chini ya Ole Gunnar Solskjaer, ambapo ukosefu wa mafanikio kama ule wa Europa Ligi ulimwacha bila kinga matokeo yalipomuendea kombo na akatimuliwa.

Amorim anakabiliwa na maamuzi magumu kuhusu kikosi chake. Wachezaji kama Lindelof na Eriksen huenda wakaondoka, huku mustakabali wa Garnacho, Mainoo na Fernandes ukiwa na sintofahamu.

Lakini ukweli ni kwamba, Amorim atalazimika kubaki na wachezaji wengi aliowategemea huko Bilbao na wengi wao, kwa uwazi, si wa kiwango cha juu.

Ufitinema Aime Gerard

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *