Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu: Rodrygo kumrithi Son Spurs?
Tottenham wanaonyesha nia ya kumsajili winga wa Real Madrid na Brazil, Rodrygo, 24, kama mbadala wa mshambuliaji wao kutoka Korea Kusini, Son Heung-min, 33. (AS – in Spanish)
Manchester United wako tayari kutoa ofa ya kwanza inayofanana na Newcastle kwa ajili ya mshambuliaji wa RB Leipzig na Slovenia, Benjamin Sesko, 22. (Sky Sports Germany)
Newcastle pia wanataka kumchukua mshambuliaji wa Paris St-Germain na Ureno, Goncalo Ramos, 24, ikiwa mpango wa Sesko utashindikana. (Daily Mail)
CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES
Inter Milan wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Manchester United na Uingereza, Mason Greenwood, 23, kutoka klabu ya Ufaransa ya Marseille. (Corriere Dello Sport – in Italian)
Klabu ya Ujerumani ya RB Leipzig iliulizia kuhusu winga wa Uingereza, Tyrique George, 19, wakati wa mazungumzo na Chelsea kuhusu uhamisho wa kiungo kutoka Uholanzi, Xavi Simons, 22. (Fabrizio Romano).
Kipa wa Paris St-Germain na Italia, Gianluigi Donnarumma, 26, ana nia ya kujiunga na Manchester United. (Teamtalk)
CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES
Klabu ya Al-Hilal ya Saudi Arabia wanamfuatilia mshambuliaji wa Liverpool na Uruguay, Darwin Nunez, 26. (Athletic – subscription required)
Winga wa Manchester United na Brazil, Antony, 25, hana nia ya kuhamia Saudi Arabia na anataka kujiunga na Real Betis, ambapo alikuwa kwa mkopo msimu uliopita. (Sport – in Spanish)
Winga wa Manchester United na Argentina, Alejandro Garnacho, 21, amesema ‘kipaumbele’ chake ni Chelsea na anasubiri mazungumzo ya kuanza kuhusu uhamisho huo. (Fabrizio Romano)
