Matokeo ya uchaguzi Uganda 2026: Kura zinahesabiwa, upinzani wadai kuna wizi wa kura

Matokeo ya uchaguzi Uganda 2026: Kura zinahesabiwa, upinzani wadai kuna wizi wa kura

Shughuli za kuhesabu kura zimeanza katika baadhi ya maeneo ya Ugandalicha ya mtandao wa intaneti kuzimwa na upinzani kutoa madai ya wizi wa kura katika uchaguzi wa rais na wabunge.

“Visa vya masanduku kujazwa kura vimeripotiwa kila mahali,” alidai mgombea mtarajiwa wa urais Bobi Wine katika ujumbe kwenye mtandao wa kijamii, bila kutoa uthibitisho madai hayo.

Mamlaka haijatoa kauli yoyote kuhusu madai yake ya udanganyifu katika uchaguzi, wala madai kwamba mawakala “wengi” wa wapiga kura na wasimamizi wa chama chake cha NUP “walitekwa nyara, na wengine kufukuzwa katika vituo vya kupigia kura”.

Changamoto ya kiufundi ulifanya shughuli ya kupiga kura kucheleweshwa hadi saa baada ya mashine zinazotumiwa kuwatambua wapiga kura kwa njia ya kielektroniki kukumbwa na hilafu.

Baadhi ya watu wamehusisha changamoto hiyo na kuzimwa kwa intaneti – pamoja na ukosefu wa vifaa vya kupigia kura, na vifaa kutofika katika baadhi ya vituo kwa wakati.

Vituo vya kupigia kura vitafungwa baadaye na sio muda uliokuwa umepangwa.

Tume ya uchaguzi ilisema mtu yeyote aliyekuwa kwenye foleni kufikia saa kumi na moja jioni saa za ndani (14:00GMT) ataruhusiwa kupiga kura yake.

Hapo awali, shirika la uchaguzi liliomba msamaha kwa “matatizo ya kiufundi” na kusema maafisa walikuwa wanafanya kazi kuyasuluhisha.

Katika kinyang’anyiro cha urais, Yoweri Museveni, 81, ambaye amekuwa madarakani tangu 1986, anagombea muhula wa saba mtawalia huku akikabiliwa na changamoto kutoka kwa Bobi Wine, nyota wa muziki wa pop mwenye umri wa miaka 43.

Matokeo ya uchaguzi wa urais yanatarajiwa kutangazwa siku ya Jumamosi saa kumi jioni saa za ndani (13:00 GMT), tume ya uchaguzi imesema.

Alhamisi asubuhi, BBC ilishuhudia hali ya mfadhaiko ikiongezeka miongoni mwa wapiga kura waliokuwa wakipanga foleni katika baadhi ya vituo vya kupigia kura katika mji mkuu, Kampala.

Japo data ya waliojitokeza kushiriki mchakato huo bado haijapatikana, waandishi walishuhudia kile kilichoonekana kuwa idadi ndogo ya watu kuliko kawaida, na hali ya kutojali miongoni mwa wapiga kura.

Wapiga kura wanakusanyika karibu na dawati wakizungumza na maafisa wa uchaguzi mjini Kampala

CHANZO CHA PICHA, AFP VIA GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, Wapiga kura katika baadhi ya maeneo ya Kampala, walipata vituo vya kupigia kura bado havijafunguliwa saa chache baada ya upigaji kura kuanza

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Baadhi ya watu waliripotiwa kuondoka katika vituo vya kupigia kura bila kupiga kura, wakisema hawawezi kusubiri changamoto za kiufundi kutatuliwa.

Mkuu wa uchaguzi Simon Byabakama aliamuru matumizi ya sajili ya kitaifa ya wapiga kura katika vituo ambavyo mashine za kibayometriki zilishindwa kufanya kazi.

Changamoto hiyo ilionekana kuathiri maeneo yote yanayoonekana kuwa na uungwaji mkono mkubwa wa serikali pamoja na yale yanayosadikiwa kuwa ngome za upinzani.

“Nina hasira kwa sababu sijapiga kura mpaka sasa. Upigaji kura ulitarajiwa kuanza kuanza saa moja, lakini hadi sasa saa mbili hatujaanza. Karatasi za kupigia kura hata hazipo, sina hata la kusema,” Kaweesi Ismail, mpiga kura mjini Kampala, aliiambia BBC.

Akipiga kura yake katika Kijiji alichozaliwa cha Rwakitura katika mkoa wa Mbarara magharibi, Rais Museveni alisema pia alipata matatizo.

“Niliweka alama ya kidole gumba kwenye mashine lakini haikukubali. Hata hivyo uso wangu ulikubaliwa papo hapo na mashine. Mashine inafanya kazi,” alisema.

Alipoulizwa kama atakubali matokeo ya uchaguzi, rais alisema: “Hii ni moja wapo wa njia za udanganyifu – inabidi tujue ni kwa nini, tatizo lilikuwa nini?”

“Sasa tunathibitisha ikiwa hii ilikuwa ya njama,” aliongeza.

,

CHANZO CHA PICHA, REUTERS

Kura ya maoni ya urais inaashiri kuwa uchaguzi huu na mbio za farasi wawili kati ya Museveni na Wine, lakini ikizingatiwa kuwa rais ameshinda chaguzi sita zilizopita, wachambuzi wanasema huenda akaongeza muda wake madarakani.

Wine ameahidi kukabiliana na ufisadi na kuleta mageuzi makubwa, huku Museveni akihoji kuwa yeye ndiye mdhamini pekee wa utulivu na maendeleo nchini.

Kipindi cha kampeni kilikumbwa na purukushani huku shughuli za upinzani zikivurugwa mara kwa mara – vikosi vya usalama vimeshutumiwa kwa kuwashambulia na kuwaweka kizuizini wafuasi wa Bobi Wine.

Msemaji wa polisi Kituuma Rusoke alipuuzilia mbali malalamishi hayo, akiwashutumu wafuasi wa upinzani, hasa wale wa chama cha Wine cha National Unity Platform (NUP) kuwa wasumbufu.

Mtandao wa intaneti ulizimwa siku ya Jumanne, huku Tume ya Mawasiliano ya Uganda ikisema hatua hiyo ilichukuliwa ili kuzuia taarifa ghushi, ulaghai na uchochezi wa ghasia – Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa Iimelaani hatua hiyo na kuelezea kuwa “inatia wasiwasi sana”.

Ufitinema Aime Gerard

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *