Mke wa Bobbi Wine aeleza mateso aliyoyapitia alipovamiwa nyumbani

Mke wa Bobbi Wine aeleza mateso aliyoyapitia alipovamiwa nyumbani

Mke wa kinara wa chama cha upinzani cha NUP nchini Uganda Bobbi Wine, Barbie Kyagulanyi ameeleza ‘mateso ‘ aliyoyapitia mikononi mwa watu anaodai ni maafisa wa usalama.

Bi Kyalunayi ambaye amelazwa katika hospitali moja mjini Kampala Uganda amesema kwamba, ‘ Ninajipa nguvu na kumuomba mume wangu asitoke mafichoni,’ alipohojiwa na wanahabari.

Wine amekuwa akiwaarifu wafuasi wake na dunia katika ukurasa wake wa mtandao wa X mcha wa Jumamosi jinsi maafisa wa usalama waliovalia barakoa walivyoivamia nyumba yake na kuharibu vitu kabla ya kuwachapa waliokuwa ndani akiwemo mke na watoto wake.

Awali Wine alihisi kuhofia usalama wa mke wake ambaye alisema alikuwa amefungiwa katika chumba kimoja na wala hakujua madhumuni ya maafisa hao yalikuwa yapi.

Barbie Kyagulanyi ambaye alizungumza kwa lugha ya Luganda alisisitiza kwamba , ‘ikiwa wanadhani kwamba watakupata mume wangu kupitia kunidhulumu mimi, basi salia mafichoni.

Jitokeze tu kwa sabbau nyinginezo na wala sio kwa sababu yangu mimi, kwani mimi niko salama na ninajipa nguvu.’Afisa Mkuu katika chama cha NUP, Mbunge Joel Ssenyonyi alichapisha ujumbe kwenye ukurasa wake wa X na kusema kwamba alifika katika makazi ya kinara wa chama chake huko Magere kuelewa zaidi kinachoendelea huko, baada ya kufahamishwa kwamba jeshi la Uganda lilikuwa limeingia ndani ya nyumba yake .

“Kuna makumi ya wanajeshi nje na wengine ambao wanaonekana wakiwa ndani ya nyumba. Baadhi wamevalia sare rasmi za kijehsi na wengie wamevalia nguo za kiraia.,” SSenyonyi alisema na kuendela kutaja kwamba alikuwa amezuiliwa kuingia ndani ya boma hilo na watu waliokuwa wamebeba silaha.

Uongozi wa chama cha NUP umesema kwamba umezungumza na maafisa wakuu wa polisi kutaka kujua ni kwa nini hatua kama hiyo dhidi ya mke wa Wine zinaendelea kuchukuliwa badala ya wao kutoa tangazo rasmi la kumtaka Wine mwenyewe au mke wake kujiwasilisha katika kituo chochote cha polisi nchini humo.

Wine amedai kwamba mke huyo alizuiliwa na mafisa waliokuwa wamebeba bunduki na kwamba walitaka kujua anapojificha kwa sasa.

‘Walichukuwa simu ya mke wangu na kumtaka kuwapa nenosiri la kuifungua siku hiyo,’ Wine aliandika kwenye mtandao wa kijami wa X.

Amedai kwamba alipokataa kuwapa walichokitaka, Wanaume hao walimpiga na kumuumiza mke wake Barbie.Mke huyo kwa sasa anendelea kupokea matibabu hospitalini akisema kwamba ana majeraha ya mwili na kiakili kutokana na alichokipitia.

Polisi hadi sasa hawajalizungumzia suala hilo wala kujibu madai yaliyotolewa na Wine, mke wake wala chama cha NUP.

Ufitinema Aime Gerard

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *