Tetesi za Soka Ulaya: Rodrygo kuondoka Madrid?Barca, Juve zamtaka Ederson

Tetesi za Soka Ulaya: Rodrygo kuondoka Madrid?Barca, Juve zamtaka Ederson

Mshambuliaji wa Brazil Rodrygo, mwenye umri wa miaka 24, anafikiria kuondoka Real Madrid katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi baada ya kupoteza nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Bernabeu. (Radio Marca)

Manchester United na Juventus wanachuana kuwania saini ya kiungo wa kati wa Brazil, Ederson mwenye umri wa miaka 25 kutoka Atalanta. (Tuttosport)

Mshambuliaji wa England Harry Kane ameendelea kuhusishwa na kurejea Ligi Kuu England, lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 anapanga kusalia Bayern Munich kwa mwaka mmoja zaidi. (Talksport)

Mlinda mlango wa Aston Villa na Argentina Emiliano Martinez, mwenye miaka 32, pamoja na winga wa Jamaica Leon Bailey, 27, wanawindwa na vilabu vya Saudi Arabia. (Telegraph)

Emiliano Martinez

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, Emiliano Martinez

Bayern Munich wanaamini wako katika nafasi nzuri ya kumsajili kiungo mshambuliaji wa Ujerumani Florian Wirtz kutoka Bayer Leverkusen, ambaye anaweza kuuzwa kwa klabu nyingine iwapo atataka kuondoka. (Sky Sports Germany)

Kocha wa zamani wa Manchester United Erik ten Hag yuko kwenye orodha ya Bayer Leverkusen ya makocha wanaoweza kumrithi Xabi Alonso, ambaye anahusishwa na kuchukua nafasi ya Carlo Ancelotti huko Real Madrid. (Sky Sports Germany)

Kiungo mshambuliaji wa England Harvey Elliott, mwenye miaka 22, amekuwa na wakati mgumu kupata nafasi ya kucheza Liverpool msimu huu lakini anataka kubaki na kupambana kwa ajili ya nafasi yake. (Liverpool Echo)

Erik ten Hag

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, Erik ten Hag

Everton ni miongoni mwa vilabu vinavyomuwinda mshambuliaji wa Ipswich Town, Liam Delap mwenye miaka 22, ambaye anaaminiwa kuwa na kipengele cha kuuzwa kwa pauni milioni 30. Wakati huo huo, uwezekano wa mshambuliaji wa England Dominic Calvert-Lewin, 28, kusaini mkataba mpya na klabu hiyo haujatupiliwa mbali. (The i Paper)

Beki wa Korea Kusini Kim Min-jae anasema anatumai atasalia Bayern Munich, ingawa klabu hiyo inaonekana kuwa tayari kumuachia mchezaji huyo mwenye miaka 28 iwapo ofa nzuri itawasili. (Sport Bild)

Mshambuliaji wa Ufaransa Enzo Kana-Biyik, mwenye umri wa miaka 18, yuko mbioni kukamilisha uhamisho wake wa bure kwenda Manchester United kutoka Le Havre. (Manchester Evening News)

Kocha wa zamani wa Wolves na West Ham, Julen Lopetegui, amesaini mkataba wa kuwa kocha wa Qatar hadi Juni 2027. (Fabrizio Romano)

Ufitinema Aime Gerard

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *