Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu: Man Utd yajiunga na mbio za kumsaka Mbeumo

Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu: Man Utd yajiunga na mbio za kumsaka Mbeumo

Manchester United yajiunga na kinyang’anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa Cameroon ambaye thamani yake inakadiriwa kuwa pauni milioni 60 Bryan Mbeumo, 25, kutoka Brentford msimu huu wa kiangazi. (Telegraph – usajili unahitajika)

Arsenal wanamfuatilia mshambuliaji wa Brazil Rodrygo anayekipiga Real Madrid, huku Manchester City pia wakimtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24. (Relevo – kwa Kihispania)

Manchester City pia wanapanga kuendeleza nia yao ya kufikia makubaliano na Nottingham Forest kwa ajili ya kiungo wao wa kati wa Uingereza Morgan Gibbs-White, 25. (Fabrizio Romano)

Arsenal na Aston Villa wanamtaka mshambuliaji wa Juventus Dusan Vlahovic, 25, huku klabu hiyo ya Serie A ikitarajiwa kuitisha pauni milioni 42 kwa Mserbia huyo. (Fichajes – kwa Kihispania)

Dusan Vlahovic

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, Mshambuliaji wa Juventus Dusan Vlahovic

Everton iko tayari kumenyana na Manchester United ili kuinasa saini ya mshambuliaji wa Ipswich Muingereza Liam Delap, 22. (Teamtalk)

Manchester United iko tayari kuwasilisha dau la kumsajili mlinzi wa Barcelona na Uruguay Ronald Araujo, 26, ikiwa itafuzu kwa Ligi ya Mabingwa. (Football365)

Leeds imemuorodhesha beki wa Marseille na Argentina Leonardo Balerdi, 26, kuwa mmoja wa shabaha yao wakuu wa uhamisho wa majira ya kiangazi. (Sun)

Real Madrid iliwapeleka waska vipaji wao kuwafuatilia beki wa Bournemouth na Uhispania Dean Huijsen, 20, na beki wa Hungary Milos Kerkez, 21, wakati wa mechi yao ya Jumamosi dhidi ya Arsenal. (TBR Football)

Miamba hao wa Uhispania pia wanamnyatia beki wa Arsenal na Ufaransa William Saliba, 24, ambaye kandarasi yake na The Gunners inaendelea hadi 2027. (L’Equipe – kwa Kifaransa)

West Brom inamtaka kocha wa Tottenham Muingereza Ryan Mason, 33, kuwa meneja wao mpya. (Sun)

Mkufunzi wa Fulham Mreno Marco Silva, 47, atawania kuchukua nafasi ya Ange Postecoglou katika klabu ya Tottenham ikiwa raia huyo wa Australia mwenye umri wa miaka 59 atatimuliwa baada ya klabu hiyo kuandikisha matokeo mabaya msimu huu. (Football Insider)

 William Saliba

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, Real Madrid wanamnyatia beki wa Arsenal William Saliba

Ufitinema Aime Gerard

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *