Je, Arsenal ni fungu la kukosa?

Je, Arsenal ni fungu la kukosa?

Nina swali hapa,Arsenal imeshinda mataji mangapi ya Klabu Bingwa Ulaya?

Ukweli sahihi ni kwamba, haijawahi kushinda hata mara moja.

Hii ikiwa Nusu Fainali yao ya kwanza tangu mwaka 2009, Arsenal imewaacha mashabiki wake wakisononeka kwa hasira na machungu kwa mara nyingine tena.

Hii ni baada ya timu yao kufurushwa tena kwenye Nusu Fainali ya Klabu Bingwa Ulaya.

Waliambulia kibano cha 2-1 dhidi ya PSG ya Ufaransa ndio ikawa mwisho wa safari yao ya michuano hiyo msimu huu.

Historia imejirudia tena..Bila shaka!

Sasa hii si mara ya kwanza kwa The Gunners kunyolewa na wembe huo wa kutu,wamehangaika sana na ukame wa kombe hili kwa miaka na mikaka.

Licha ya kuwa ni timu kigogo katika Ligi Kuu ya Soka ya England, wamekuwa na mafanikio kiduchu sana michuano ya Ulaya. Kombe hili linawatesa.

Wamefika mara moja pekee katika fainali,na hawakufua dafu dhidi ya Barcelona mwaka 2006,walifungwa 2-1, mwisho wa habari.

Hebu tuangazie mikosi ya nusu fainali,Arsenal walifika hatua hiyo mara tatu tu.

Mwaka huu 2025 na mara ya mwisho mwaka 2009 walipochezea sharubu za babu dhidi ya Manchester United baada ya kutitigwa mabao 4-1.

Hali kadhalika,wanabunduki hawa pia wamekutana na milima na mabonde katika hatua za robo fainali,Arsenal walititigwa mara 7 katika mechi 8 za robo fainali zilizopita, ikiwemo mara nne mtawalia katika miaka 9.

Si hayo tu,Arsenla pia imejipata kwenye mshike mshike katika hatua ya raundi ya 16,wamewahi kuyaaga mashindnao hayo mara sita mtawalia hatua hiyo..Kuanzia mwaka 2011 hadi 2016 kila mwaka walighadhabishwa katika hatua hiyo.Mwaka 2015 walitupwa nje ya raundi ya 16 dhidi ya Monaco licha ya kutoka sare ya mabao 3-3 ,hii wakijipata hasarani kwa goli la ugenini.Hali hii ikajuridia tena mwaka 2016 walipotolewa tena na Fc Barcelona.

Arsenal ilikuwa inatazamia kutinga fainali yao ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa baada ya miaka 19

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, Arsenal ilikuwa inatazamia kutinga fainali yao ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa baada ya miaka 19

Tukiachana na Klabu Bingwa Ulaya, kwani huko Ligi Kuu ya England kunasemaje?

Arsenal imeshinda taji hilo mara 13,lakini je, mara ya mwisho ni lini? Miaka 21 iliyopita? Piga mstari miaka 21.

Mara ya mwisho Arsenal kunyakuwa ligi kuu nchini England ni mwaka 2004 ,walishinda ligi hiyo bila kufungwa hata mechi moja wakiwa na kocha Arsene Wenger, lakini hii sherehe hiyo iligeuka kama nuksi kwao, kwani kutoka hapo hawajaligusa tena kombe hilo kwa miaka 21. Wamebaki wakilitazama na kulimezea mate tu.

Hizi hapa takwimu za mataji mengine ambayo Arsenal wana kiu nayo.

Hawakashinda kombe la carabao kwa miaka 33,hawashinda kombe la Europa hata mara moja,hawajashinda katu Uefa super cup na kombe la klabu bingwa duniani hawalikaribia pia.

Yote tisa hilli kombe la Klabu Bingwa Ulaya ndio sumu yao iliyo uchungu kama subili, hawajalishinda kwa miaka 139 tangu lianzishwe,kwa Arsenal imebaki stori ya miaka nenda miaka rudi kama tamthilia ya jinamizi isiyoisha.

Ufitinema Aime Gerard

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *