Mtu mwenye damu yenye uwezo wa kukabiliana na sumu ya nyoka

Mtu mwenye damu yenye uwezo wa kukabiliana na sumu ya nyoka

Damu ya mwanamume wa Marekani ambaye alijidunga sumu ya nyoka kimakusudi kwa takriban miongo miwili imesababisha kugunduliwa kwa dawa “isiyo na kifani”, wanasema wanasayansi.

Kingamwili zinazopatikana katika damu ya Tim Friede zimeonyeshwa kulinda dhidi ya sumu kutoka kwa aina mbalimbali za wanyama.

Matibabu ya sasa yanapaswa kuendana na aina maalum ya sumu ambayo mtu huyo ameumwa nayo.

Lakini misheni ya Bw Friede ya miaka 18 inaweza kuwa hatua muhimu katika kutafuta dawa ya kimataifa dhidi ya sumu ya nyoka – ambayo inaua hadi watu 140,000 kwa mwaka na kuacha mara tatu ya wengi wanaohitaji kukatwa viungo au kukabiliwa na ulemavu wa kudumu.

Kwa jumla, Bw Friede amevumilia kuumwa zaidi ya mara 200 na zaidi ya sindano 700 za sumu alizotayarisha kutoka kwa baadhi ya nyoka wabaya zaidi kote duniani, wakiwemo aina nyingi wa mamba, cobra, taipan na kraits.

Hapo awali alitaka kujenga kinga yake ili kujilinda anaposhika nyoka, akiandika ushujaa wake kwenye YouTube.

Lakini fundi huyo wa zamani wa lori alisema kuwa alijipata katika hali ya taabani wakati nyoka wawili aina ya cobra walipomshambulia na kumng’ata akimwacha katika hali ya kukosa fahamu.

“Sikutaka kufa. Sikutaka kupoteza kidole. Sikutaka kukosa kazi,” aliambia BBC.

Motisha ya Bw Friede ilikuwa kuendeleza matibabu bora zaidi kwa ulimwengu wote, akieleza: “Ikawa mtindo wa maisha na niliendelea tu kusukuma na kusukuma na kusukuma kwa nguvu niwezavyo – kwa watu ambao wako umbali wa maili 8,000 kutoka kwangu ambao hufa kutokana na majeraha ya nyoka”.

‘Ningependa kupata damu yako’

Dawa ya kutibu sumu ya nyoka hutengenezwa kwa kudunga dozi ndogo za sumu ya nyoka ndani ya wanyama, kama vile farasi. Mfumo wao wa kinga hupambana na sumu kwa kutoa kingamwili na hizi huvunwa ili kutumika kama tiba.

Lakini sumu yenyewe na dawa ya kuuwa sumu hiyo lazima zilinganishwe kwa karibu kwa sababu sumu ya nyoka anayekung’ata hutofautiana kutoka kwa spishi ya nyoka mmoja hadi nyingine.

Kuna hata aina mbalimbali ndani ya spishi zile zile – kwa mfano antivenom iliyotengenezwa kutoka kwa nyoka nchini India haina ufanisi dhidi ya spishi zile zile ya nyoka nchini Sri Lanka.

Timu ya watafiti ilianza kutafuta aina ya ulinzi wa kinga inayoitwa kingamwili kwa upana. Badala ya kulenga sehemu ya sumu inayoifanya kuwa ya kipekee, wanalenga sehemu ambazo ni za kawaida kwa aina zote za sumu.

Hapo ndipo Dk Jacob Glanville, mtendaji mkuu wa kampuni ya kibayoteki ya Centivax, alipokutana na Tim Friede.

“Mara ya kwanza nilijiambia iwapo kuna mtu yeyote ulimwenguni ameunda kingamwili hizi za kupunguza kwa kiasi kikubwa, atakuwa yeye’ na kwa hivyo niliwasiliana naye,” alisema.

“Simu ya kwanza, nilisema ‘hii inaweza kuwa ngumu, lakini ningependa kupata damu yako’.”

Bw Friede alikubali na kazi hiyo ikapewa kibali cha kimaadili kwa sababu utafiti huo ungechukua damu tu, badala ya kumpa sumu zaidi.

.

CHANZO CHA PICHA, JACOB GLANVILLE

Maelezo ya picha, Tim Friede, katikati, alitaka kusaidia kuendeleza matibabu bora kwa waathiria wa majeraha ya nyoka

Utafiti ulilenga elapids – moja ya familia mbili za nyoka wenye sumu – kama vile nyoka wa matumbawe, mamba, cobra, taipan na kraits.

Elapids kimsingi hutumia sumu ya niuro katika sumu yao, ambayo hulemaza mwathiriwa wake na ni mbaya wakati inasimamisha misuli inayohitajika kupumua.

Watafiti walichagua aina 19 za elapidi zilizotambuliwa na Shirika la Afya Ulimwenguni kuwa miongoni mwa nyoka hatari zaidi duniani. Kisha wakaanza kupekua damu ya Bw Friede ili kupata ulinzi.

Kazi yao, iliyofafanuliwa katika jarida la Cell, ilibainisha kingamwili mbili ambazo zinaweza kulenga aina mbili za sumu ya neva. Waliongeza katika dawa ambayo inalenga theluthi moja kutengeneza cocktail yao ya antivenom.

Katika majaribio ya panya, machanganyiko huo wa dawa ya kukabiliana na sumu ya nyoka ulimaanisha kuwa wanyama hao walinusurika katika kipimo cha vifo kutoka kwa spishi 13 kati ya 19 za nyoka wenye sumu. Walikuwa na ulinzi wa sehemu dhidi ya sita waliosalia.

Huu ni upana “usio na kifani”, kulingana na Dk Glanville, ambaye alisema “huenda inashughulikia rundo zima la elapidi ambazo hazina dawa dhidi yake .”

.

CHANZO CHA PICHA, JACOB GLANVILLE

Maelezo ya picha, Watafiti wanaofanya kazi katika kuunda dawa moja itakayokabiliana na sumu ya nyoka

Timu inajaribu kuboresha kingamwili zaidi na kuona ikiwa maboresho zaidi yanaweza kusababisha ulinzi kamili dhidi ya sumu ya nyoka.

Aina nyingine ya nyoka – nyoka – hutegemea zaidi haemotoxins, ambayo hushambulia damu, badala ya neurotoxini. Kwa jumla kuna takriban aina dazeni ya sumu za nyoka, zikiwemo cytotoxins ambazo huua seli moja kwa moja.

“Nadhani katika miaka 10 au 15 ijayo tutakuwa na kitu cha ufanisi dhidi ya kila tabaka la sumu,” alisema Prof Peter Kwong, mmoja wa watafiti katika Chuo Kikuu cha Columbia.

Na utafiti unaendelea ndani ya sampuli za damu za Bw Friede.

“Kingamwili za Tim ni za ajabu sana – alifundisha mfumo wake wa kinga kupata utambuzi huu mpana,” alisema Prof Kwong.

Tumaini kuu ni kuwa na dawa ya sumu ya nyoka ambayo inaweza kufanya kila kitu, au sindano moja ya elapidi na moja ya nyoka.

Prof Nick Casewell, ambaye ni mkuu wa kituo cha utafiti na uingiliaji kati wa kuumwa na nyoka katika Shule ya Liverpool ya Madawa ya Kitropiki, anasema upana wa ulinzi unaoripotiwa “hakika una”ushahidi wa nguvu” kwamba hii ilikuwa mbinu inayowezekana.

“Hakuna shaka kuwa kazi hii ni hatua kubwa katika mwelekeo wa kusisimua.”

Lakini alionya kwamba kulikuwa na “kazi nyingi za kufanya” na kwamba antivenom bado inahitaji majaribio ya kina kabla ya kutumika kwa watu.

Lakini kwa Bw Friede, kufikia hatua hii “hunifanya nijisikie vizuri”.

“Ninafanya kitu kizuri kwa ubinadamu na hiyo ilikuwa muhimu sana kwangu. Ninajivunia. Ni hatua nzuri sana.”

Ufitinema Aime Gerard

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *