Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi: Liverpool, Barca, Madrid zamgombania Wharton

Liverpool wanatarajiwa kupambana na Real Madrid na Barcelona kumsaka kiungo wa Crystal Palace na timu ya taifa ya England, Adam Wharton, mwenye umri wa miaka 21 na anayekadiriwa kugharimu £60m. (Daily Mail)
Uhamisho wa mshambuliaji wa Chelsea raia wa Ufaransa, Christopher Nkunku, mwenye umri wa miaka 27, unaweza pia kuwa sehemu ya mipango ya majira ya kiangazi ya Liverpool. (Footmercato)
Klabu tatu za Ligi Kuu ya England, Chelsea, Manchester City na Arsenal tayari zimefanya mazungumzo na mawakala wa mshambuliaji wa Real Madrid raia wa Brazil, Rodrygo, mwenye umri wa miaka 24, ambaye hana namba katika kikosi cha kwanza cha Bernabeu. (Fichajes)

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES
Wolves wanazidisha juhudi zao kumsajili kiungo wa Liverpool raia wa England, Harvey Elliott, mwenye umri wa miaka 22. (GiveMesport)
Aston Villa wanatumaini kufanya uhamisho wa kudumu wa beki wa Chelsea, Axel Disasi, raia wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 27, na tayari wameanza mazungumzo. (Footmercato)
Chelsea, kwa upande mwingine, wana orodha ya wachezaji wa kusajili enelo la mabeki wa kati, wakiwemo Jarrad Branthwaite, Mwingereza mwenye umri wa miaka 22 wa Everton, na Marc Guehi, 24, wa Crystal Palace ambaye pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya England. (Sky Sports)

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES
Aston Villa wanaweza kumrudisha mshambuliaji wa Barcelona, Ferran Torres, raia wa Hispania mwenye umri wa miaka 25, katika Ligi Kuu ya England kwa ada inayokadiriwa kuwa £42m katika dirisha la usajili la kiangazi. (Birmingham Mail)
Southampton wanavutiwa na beki wa kulia wa Sturm Graz, Max Johnston, mwenye umri wa miaka 21 na ambaye ni raia wa Scotland, ambaye anaripotiwa kuwa anapatikana kwa £3m. (Sky Sports)
Wrexham wanatafakari kumsajili kiungo wa Nottingham Forest, Lewis O’Brien, mwenye umri wa miaka 26 kwa sasa yuko kwa mkopo Swansea City kufuatia kupanda Championship. (Football League World)