Simba yashindwa kufurukuta fainali

Klabu ya Morocco – RS Berkane imetawazwa mabingwa wa Kombe la Shirikisho la CAF kwa mara ya tatu baada ya sare ya 1-1 ugenini dhidi ya Simba SC na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa jumla ya 3-1 katika fainali iliyochezwa Jumapili kisiwani Zanzibar
Simba ilijipa matumaini kwa bao la mapema la Joshua Mutale dakika ya 17, lakini kasi ya upande wa Tanzania ilidhibitiwa baada ya beki Yusuf Kagoma kutolewa nje kwa kadi nyekundu dakika tano za kipindi cha pili.
Berkane ilionyesha uzoefu zaidi katika mechi hiyo na ilitawala nyakati muhimu wa mechi katika awamu zote mbili.
Licha ya klabu ya SC Simba kuonyesha mchezo mzuri na ari ya kutaka kushinda, Berkane ilionyesha mchezo wa kiwango cha juu zaidi kwa Simba kumudu .

CHANZO CHA PICHA, SIMBA SC/X
Uwanja wa Amaan ulijaa tafrani huku Simba wakifunga bao la pili baada ya Steven Mukwala kufunga kwa kichwa kizuri kilichompita kipa Munir Mohamed.
Hatahivyo mashabiki hao walinyamazishwa dakika chache baadaye baada ya VAR kusema kwamba alikuwa ameotea .
Taji hilo linaashiria ushindi wa tatu wa RS Berkane wa Kombe la Shirikisho la CAF katika kipindi cha miaka mitano, na hivyo kuimarisha sifa yao kama moja ya vilabu vyenye msimamo thabiti katika misimu ya hivi karibuni.
Renaissance Berkane ilifanikiwa kufuzu kwa fainali ya Kombe la Shirikisho baada ya kuitoa timu ya Algeria, CS Constantine, katika nusu fainali kwa jumla ya mabao (4-1) huku Simba ikifuzu kupitia mikwaju ya penalti baada ya kutoka sare ya 2-2 dhidi ya klabu ya Al-Masry ya Misri ..