Wanaume wa aina gani wako hatarini zaidi kupata saratani ya tezi dume?

Wanaume wa aina gani wako hatarini zaidi kupata saratani ya tezi dume?

Saratani ya tezi dume ziko za aina tofauti. Baadhi huenea haraka, huku nyingine hukua polepole na huhitaji ufuatiliaji na matibabu.

Tezi dume ni tezi iliyoko chini ya kibofu cha mkoji cha wanaume. Ni mrija unaobeba mkojo kutoka kwenye kibofu hupitia katikati ya tezi dume.

Saratani ya tezi dume kama zilivyo saratani nyingine, ni ukuaji usio wa kawaida wa seli. Saratani hii hutokea kama uvimbe fulani au uvimbe unaokuwa polepole.

Saratani ya tezi dume kwa wanaume lazima igunduliwe na kuzuiwa mapema, kwani baadhi ya aina za saratani hukua haraka na zinaweza kusababisha kifo.

Saratani ya tezi dume ikigunduliwa mapema, ina nafasi kubwa ya kupatiwa matibabu yenye mafanikio.

Saratani ya tezi dume kwa nchini Uingereza hugunduliwa kwa mwanaume mmoja kati ya wanane. Saratani hii huwapata zaidi wanaume wazee wenye umri wa zaidi ya miaka 75. Ni nadra sana kwa wanaume walio chini ya umri wa miaka hamsini.

Historia ya familia pia inahusika. Ikiwa mwanafamilia au jamaa wa karibu, kama vile baba yako, babu, au mjomba wako, amewahi kuwa na saratani ya tezi dume, hatari yako ya kupata ugonjwa huo pia ni kubwa.

Uchunguzi unaonyesha wanaume wenye ngozi nyeusi wana uwezekano mkubwa wa kuathiriwa na ugonjwa huu.

Dalili, vipimo na matibabu

Dalili za kawaida za saratani ya tezi dume ni pamoja na:

  • Wagonjwa wa saratani hii hukojoa mara kwa mara, hasa usiku.
  • Kuwa na tatizo la mtiririko wa mkojo polepole sana.
  • Mkojo unakuwa na damu na maumivu sawa na kisonono.
  • Dalili hizi zinaweza kusababishwa na matatizo mengine, lakini unapaswa kumwona daktari ikiwa unaona mabadiliko yoyote katika mkojo wako.

Madaktari hugundua ugonjwa huo kwa njia tofauti. Njia moja ya kuitambua ni kupitia kipimo cha damu na skana ya MRI. Sindano huingizwa kwenye kibofu na seli hutolewa kwa ajili ya uchunguzi. Lakini utafiti unaonyesha uchunguzi kupitia MRI ni bora zaidi.

Madaktari wanapendekeza ikiwa unataka kufanya kipimo cha njia ya damu, unapaswa kuepuka ngono na mazoezi ya nguvu siku mbili kabla, kwani hayo yanaweza kuathiri matokeo ya kipimo.

Kuna njia tofauti za kutibu. Daktari wako anaweza kukupa ushauri bora na unaofaa zaidi.

Ikiwa saratani iko katika hatua zake za mwanzo na haina dalili na inakua polepole, inaweza kufuatiliwa na kusubiriwa ikue kidogo.

Baadhi ya vimbe zinaweza kutibiwa kwa upasuaji na mionzi.

Tiba ya homoni pia inaweza kupunguza kasi ya ukuaji wa saratani.

Matibabu ya cryotherapy huzuia ukuaji wa seli za kansa na kuharibu uvimbe.

Ufitinema Aime Gerard

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *