Tetesi za soka Ulaya Jumanne: Man Utd kuanza mazungumzo na Mbeumo

Mshambulizi wa Brentford Bryan Mbeumo anataka kujiunga na Manchester United , ambayo sasa iko tayari kuanzisha mazungumzo ya kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Cameroon mwenye umri wa miaka 25. (Subscription requires)
Inter Milan wanatumai kumsajili mshambuliaji wa Manchester United na Denmark Rasmus Hojlund, 22, kwa mkopo msimu huu. (Gazzetta dello Sport – In Italic)

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES
Manchester United pia inasubiri uamuzi kutoka kwa kiungo wa kati wa Ureno Bruno Fernandes kuhusu kama anataka kusalia katika klabu hiyo au kuondoka, huku klabu ya Saudi Arabia Al-Hilal ikimtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30. (Sky Sports)
Mshambulizi wa Crystal Palace Mfaransa Jean-Philippe Mateta, 27, pia yuko kwenye orodha ya washambuliaji wa Manchester United , lakini huenda wakakabiliwa na ushindani kutoka kwa Juventus na AC Milan . (TeamTalk)

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES
Myles Lewis-Skelly, 18, anatarajiwa kusaini kandarasi mpya na Arsenal msimu huu wa kiangazi, huku The Gunners wakiwa na nia ya kuzuia tetesi za kutaka kumnunua beki huyo wa Uingereza kutoka Real Madrid . (Mirror)
Liverpool wamekubali mkataba na kiungo wa kati wa Ujerumani Florian Wirtz hadi 2030, lakini bado hawajakubali ada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22, huku Bayer Leverkusen wakikataa ofa ya euro 130m (£110m) kutoka kwa Reds huku wakishikilia euro 150m (£127m). (Bild – in German)

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES
Barcelona wameanza mazungumzo ya awali na winga wa Liverpool Luis Diaz, 28, wakimtaka Saudi Arabia kumnunua mchezaji huyo wa Colombia. (Florian Plettenberg)
Chelsea wanafikiria kumnunua mlinzi wa kati wa Everton na England Jarrad Branthwaite, 22, wakati Tottenham wanaweza kushindana na The Blues kuwania saini yake msimu huu wa kiangazi. (TeamTalk)
Kiungo wa kati wa Uingereza Jobe Bellingham amechagua kujiunga na klabu ya zamani ya kaka yake Jude Borussia Dortmund badala ya Eintracht Frankfurt na RB Leipzig na klabu hiyo ya Ujerumani itaanza mazungumzo na Sunderland kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19. (Bild – in Germany)

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES
Manchester City wanakaribia kufikia makubaliano ya kumnunua kiungo wa kati wa AC Milan na Uholanzi Tijjani Reijnders, 26, kwa ajili ya Kombe la Dunia la Klabu la Fifa litakaloanza Juni 14 nchini Marekani. (Football Italia)
Chelsea pia wanafikiria kumnunua winga wa Borussia Dortmund Muingereza Jamie Gittens, 20, ambaye anaweza kugharimu takriban £50m. (Guardian)
Everton, Manchester United na West Ham wanaweza kumnunua mshambuliaji wa Serbia Aleksandar Mitrovic, huku Al-Hilal wakiwa tayari kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30. (Sport)

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES
Kiungo wa kati wa zamani wa Arsenal na England Jack Wilshere, 33, ndiye mtangulizi wa kuwa meneja wa League One Plymouth Argyle . (Sun)
Brighton wanafuatilia mwenendo wa kiungo wa kati wa Sheffield United Ollie Arblaster, 21, anapoendelea kupata nafuu kutokana na jeraha . ( TeamTalk )