Fahamu faida ya aloe vera kwa afya

Aloe Vera ni mmea wa kijani kibichi, ambao hukua katika hali ya hewa yenye joto. Chanzo chake cha afya kinahusiana na jeli ambayo hutolewa ndani ya majani yake.
Ingawa mmea huu unakuzwa ulimwenguni kote kwa sababu ya umaridadi wake na uwezo wake wa kutibu magonjwa, chimbuko lake ni Afrika.
Afrika Kusini ndio kitovu cha aloe vera ikiwa na zaidi ya aina 120 za mmea huo.
Mmea wa aloe vera unajumuisha zaidi ya viungo 75 vinavyofanya kazi, ikiwa ni pamoja na vimeng’enya, asidi ya amino, vitamini, na madini, na baadhi ya vitu hivyo vinaweza kutumiwa kutibu magonjwa.
Matumizi ya Aloe Vera
1. Inakabiliana na bakteria
Aloe vera inajulikana kupambana na virusi, kuua vimelea na viini. Na hii ndio sababu moja inayofanya iwe rahisi kuponya majeraha na kutibu matatizo ya ngozi.
Mmea huu pia huzuia bakteria mbalimbali kukua, na bakteria zilizochunguzwa zaidi ni Staphlococcus aureus na Pseudomonas aeruginosa zenye kuathiri ngozi.
2. Inaharakisha uponyaji wa majeraha
Mara nyingi watu hutumia aloe vera kama dawa ya kutibu magonjwa kwa kuinyunyiza kwenye ngozi badala ya kuinywa.
Uchunguzi unaonyesha kwamba ni tiba nzuri kwa ajili ya majeraha ya kuungua ya kiwango cha kwanza na cha pili.
Kwa mfano, mapitio ya majaribio yaliofanywa na jarida moja linaloaminika ulionyesha kwamba aloe vera inaweza kupunguza muda wa uponyaji wa majeraha ya moto kwa siku 9 ikilinganishwa na dawa za kawaida.
Pia inasaidia kuzuia kuwasha na maambukizo.
Uthibitisho wa kwamba aloe vera husaidia kuponya aina nyingine za majeraha hauwezi kuthibitishwa, lakini utafiti huo unaonyesha kuna matumaini.
3. Inapunguza ukoga wa meno
Kuoza kwa meno na magonjwa ya fizi ni tatizo la afya la kawaida sana. Mojawapo ya njia bora zaidi za kuzuia hali hizo ni kupunguza kuongezeka kwa ukoga, au bakteria zilizo kwenye meno.
Katika utafiti uliofanyiwa wanafunzi 152 wenye umri wa kati ya miaka 8 na 14, watafiti walilinganisha dawa ya kusukutua mdomo inayotokana na aloe vera na chlorhexidine inayotumiwa kutengeneza dawa ya kusukutua mdomo.
Baada ya kutumia dawa hiyo kwa majuma 4, ilipunguza ukoga, uvimbe wa fizi, na (bacteria inayosababisha ukoga) kwenye mate, na hivyo ikawa sawa na dawa ya chlorhexidine.
Utafiti mwingine wa mwaka 2021 ulihitimisha kwamba dawa ya kusukutua mdomo inayotokana na aloe vera ni njia mbadala ya asili ya dawa iliyotengenezwa kwa kemikali.
Jeli ya Aloe vera pia ni chanzo cha kuaminika katika kuua vijidudu wanaopatikana katika mdomo inayojulikana kama Candida albicans.
3. Inapunguza kuvimbiwa
CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES
Wakati huu, ni utomvu, wala si jeli unaotoka kwenye mabaki ya rangi ya manjano yenye kunata yaliyo chini ya ngozi ya jani.
Hata hivyo, utomvu una dutu inayofahamika kama aloin kwa Kiingereza ambayo inaweza kuwa na athari mbaya kama vile kusababisha maumivu ya tumbo na athari nyingine mbaya zinapotumiwa kwa kiasi kikubwa.
Kwa sababu hii, haijapatikana nchini Marekani kama dawa tangu mwaka 2002.
4. Manufaa yake kwenye ngozi
Kuna uthibitisho wa awali unaoonyesha kwamba jeli ya aloe vera inaweza kupunguza dalili za kuzeeka kwa ngozi.
- Unyevu wa ngozi
- Kuimarishwa kwa ngozi
- Pia ina kolagini
Mbali na yote hayo inaweza kuchangia kuwa na ngozi yenye afya.
5. Kupunguza viwango vya sukari ya damu
Baadhi za tafiti zilionyesha kwamba kunywa juisi ya aloe vera kunaweza kusaidia watu kufikia viwango bora vya sukari kwenye damu, na pia kupunguza mafuta na uzito wa mwili.
Wakati mwingine, watu hutumia aloe vera kama tiba ya ugonjwa wa sukari. Hii ni kwa sababu inaweza kuimarisha jinsi seli za mwili zinavyoitikia insulini na kusaidia kuboresha udhibiti wa sukari ya kwenye damu.
Jinsi ya kutumia aloe vera
Inaweza kutumiwa kwa njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na jeli au dawa ya kupaka.
Inaweza kutumiwa ikiwa mbichi, ungaunga ama ikiwa katika hali ya umajimaji.
Aloe Vera imekuwa yenye kutoa matumaini kwa wenye ugonjwa wa sukari ambao wanataka kudumisha viwango vya sukari ya damu. Lakini, wanasayansi hawajaafikia makubaliano juu ya kupendekeza Aloe Vera kama njia ya kudhibiti ugonjwa wa kisukari.
Pia, utafiti zaidi unahitajika kufanywa ili kuamua aina sahihi ya maandalizi na kipimo.
Hivyo basi, ni muhimu kuwa mwangalifu wakati unaitumia hasa kama wewe ni mgonjwa wa kisukari.
Hatari za Aloe Vera
CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES
Aloe vera, ingawa mmea huu unajulikana na wengi kama “mti usiokufa”, kwa manufaa yake mengi ya kiafya tangu karne na karne, kama dawa nyingine yoyote, pia haikosi athari zake.
Upande wa ugonjwa wa kisukari, ikiwa tayari unatumia dawa ili kudhibiti kiwango cha sukari katika damu yako, kunywa glasi kubwa ya juisi ya aloe vera au kutumia dawa nyingine ya aloe vera kunaweza kupunguza sana kiwango cha sukari katika damu yako.
Unaweza kuugua ugonjwa wa ‘hypoglycemia’, kushuka sana kwa kiwango cha sukari katika damu na inaweza kusababisha upoteze fahamu.
Watu wengine wanatumia aloe vera kama kichocheo cha kuwezesha kuhara. Kuharisha inaweza kuwa hatari ikiwa kutaendelea bila kupata matibabu kwa sababu ya upungufu wa maji mwilini.
Baadhi ya watu wanaweza kuwa wanadhurika na viungo vingine vinavyopatikana ndani ya aloe vera na hivyo, kuwa rahisi kwao kupata mzio wa ngozi kama vile uvimbe.
Usitumie aloe vera ya jeli kwenye ngozi iliyopata maambukizi. Wakati jeli ina vijiumbe-maradhi, safu yake ya kinga inaweza kuvuruga mchakato wa uponyaji na kufanya maambukizi kuwa mabaya zaidi.