“Kuna uwezekano wa kufikia makubaliano ya amani DR Congo“- Rais Kagame
Rais Paul Kagame wa Rwanda amesema kuwa kuna fursa ya kufikia makubaliano ya amani katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na kuongeza kuwa mzozo katika nchi hiyo unasababishwa na msukumo kutoka nje.
Akizungumza katika kikao na wanahabari, Kagame amesema kuwa hatua zozote za kutatua mzozo unaoendelea huko DR Congo ni lazima zijumuishe suala la FDLR.
Vile vile, Kagame aligusia juhudi za utafutaji amani za rais wa Marekani Donald Trump na kuongeza kuwa ni muhimu kwa kwa kila nchi kutekeleza wajibu wake kahakikisha ufikiaji wa amani.
“Rwanda inaunga mkono juhudi na maamuzi ya Trump kuhusu mgogoro wa DRC,” alisema Kagame.
“Mgogoro wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo unahusisha pande tatu, kisiasa, kiuchumi na msukumo wa nje,” Kagame alisema.
Kagame ametoa hakikisha la kutimiza wajibu wake katika makubaliano lakini akaongeza kuwa utekeleza wa makubaliano yoyote ni jukumu la serikali ya DR Congo.
