DRC yatangaza mlipuko wa ugonjwa wa Ebola

DRC yatangaza mlipuko wa ugonjwa wa Ebola

Takriban watu 15 wamefariki katika mlipuko mpya wa virusi vya Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wizara ya afya ya nchi hiyo imesema.

Virusi hivyo vilipatikana kwa mwanamke mjamzito mwenye umri wa miaka 34 ambaye alikuwa amelazwa hospitalini mwezi uliopita baada ya kuonyesha dalili ambazo ni pamoja na homa kali na kutapika mara kwa mara, wizara hiyo ilinukuliwa na shirika la habari la Reuters ikisema.

Alifariki tarehe 25 Agosti 2025 kbaada ya viungo kadhaa mwilini mwake kushindwa kufanya kazi.

Huu utakuwa ni mlipuko wa 16 wa virusi hivyo hatari katika taifa hilo kubwa la Afrika ya kati ambalo halina huduma imara za afya, na hukumbwa na mzozo mashariki mwa nchi hiyo.

Mlipuko wa hivi punde umeripotiwa katika jimbo la kati la Kasai, huku watu 28 wakishukiwa kuwa na maambukizi , wizara ilisema.

Kufikia sasa kuna wagonjwa 6 ambao wamewekwa chini ya uangalizi kwa kuonyesha na dalili zinazoshukiwa kuwa za ebola.

Kati ya watu 15 waliofariki, wanne walikuwa wahudumu wa afya akiwemo muuguzi na mhudumu wa maabara.

Wizara hiyo inasema huu ni mlipuko wa 16 wa Ebola nchini humo – mlipuko wa kwanza ulitokea mnamo 1976.

Ufitinema Aime Gerard

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *