Tetesi za soka Ulaya Jumatano: Tottenham Hotspur sasa yamtaka beki wa Crystal Palace Marc Guehi

Tetesi za soka Ulaya Jumatano: Tottenham Hotspur sasa yamtaka beki wa Crystal Palace Marc Guehi

Tottenham ni miongoni mwa timu zinazowania saini ya beki wa Crystal Palace na Uingereza Marc Guehi, 25. (CaughtOffside)

Meneja wa Tottenham Thomas Frank anataka kumleta mlinzi wa Jamhuri ya Ireland Nathan Collins, 24, kutoka Brentford. (TBR Football)

Kiungo wa kati wa Tottenham na Uruguay Rodrigo Bentancur, 27, anakaribia kukubaliana kandarasi mpya na klabu hiyo ya London. (Football.London)

.

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, Reuben Amorim

Habari za ndani ya Manchester United zinahofia meneja wa Ureno Ruben Amorim, 40, atajiuzulu kabla ya kutimuliwa. (iPaper)

Kiungo wa kati wa Real Madrid na Uruguay Dro Fernandez, Federico Verlvade, 27, analengwa na Manchester United mwaka ujao. (Fichajes – In Spanish).

Kiungo wa kati wa Barcelona na Uhispania Dro Fernandez, 17, hana nia ya kusikiliza ofa kutoka nje ya nchi, licha ya klabu za Arsenal, Chelsea na Manchester City kumataka. (TBR Football)

.

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, Valverde

Fulham wanapanga kumnunua kiungo wa Middlesbrough Muingereza Hayden Hackney, 23. (Football league World)

Ufitinema Aime Gerard

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *