Mkakati wa Iran wa kutumia makombora umebadilika vipi?

Mkakati wa Iran wa kutumia makombora umebadilika vipi?

Kulingana na utafiti uliofanywa na BBC Arabic, Iran imerusha makombora zaidi katika mataifa ya Ghuba baada ya kushambuliwa na Marekani na Israel, kuliko ilivyokuwa katika vita vya siku 12 dhidi ya Israel mwaka uliopita.

Kulingana na takwimu zilizotolewa na Saudi Arabia, Qatar, United Arab Emirates, Bahrain, na Kuwait, idadi ya makombora yaliyorushwa dhidi ya mataifa ya Ghuba kati ya Februari 28 na Machi 4 inazidi 550.

Oman haijatangaza idadi ya mashambulizi ya makombora na ndege zisizo na rubani walizorushiwa na Iran. Wakati huo huo, Marekani na Israel zimerusha maelfu ya mabomu dhidi ya Iran.

Rais wa Iran Masoud Pezeshkian ameomba radhi kwa mashambulizi hayo dhidi ya mataifa ya Ghuba na ameahidi kwamba kama ardhi yao haitatumika kuishambulia Iran, basi Iran pia haitawashambulia.

Mhariri wa masuala ya ulimwengu wa BBC, John Simpson, anasema kwamba ingawa Pezeshkian ametoa ujumbe wa amani, swali ni je, maneno yake yanaweza kuzingatiwa kama msimamo wa uongozi wa Iran?

Uwezo wa ulinzi wa Iran unajumuisha makombora ya balistiki na ya hypersonic, na pia ina ndege zisizo na rubani, lakini hivi karibuni imeonekana kubadilisha mkakati wake katika mashambulizi dhidi ya Israel na mataifa ya Ghuba.

Ni nini tunajua kufikia sasa kuhusu makombora haya? Nini kilicho tofauti wakati huu ikilinganishwa na vita vya awali dhidi ya Israel, na Iran inaweza kutegemea kwa kiasi gani silaha zake?

Tunachokijua kuhusu makombora haya?

.

CHANZO CHA PICHA, WISAM HASHLAMOUN/ANADOLU VIA GETTY IMAGES

Iran ina makombora ya masafa mafupi na ya kati. Kulingana na ripoti mbalimbali za taasisi za ulinzi na uchambuzi wa kimataifa, makombora ya umbali mfupi ya Iran yana uwezo wa kufika urefu wa takriban kilomita 300 hadi 1,000 ambayo inamaanisha kwamba nchi kadhaa jirani, ikiwa ni pamoja na mataifa ya Ghuba, zinaweza kufikiwa na makombora haya.

Makombora haya ya umbali mfupi na wa kati, ni sehemu ya uwezo wake wa kijeshi wa maeneo ya karibu.

Iran pia, ina makombora ya umbali wa kati ambayo yanaweza kufika umbali wa kilometa 1,000 hadi 2,000, na hivyo inaweza kufika Israel na maeneo mengine ya kimkakati katika eneo hilo.

Kwa mujibu wa takwimu mbalimbali za vyombo vya ulinzi na uchambuzi:

Shahab 1: makombora ya umbali wa takriban 300 km.

Fateh 110: makombora ya umbali wa 300 – 500 km.

Shahab 2: makombora ya umbali wa 500 km.

Zulfiqar: makombora ya umbali wa 700 km.

Qiyam 1 / Qiam 1: makombora ya umbali wa takriban 700 – 800 km.

Shahab 3: makombora ya umbali wa takriban 800 – 1,300 km.

Hii inaonyesha kwamba Iran ina mchanganyiko wa makombora ya umbali mfupi na wa kati ambayo yana uwezo wa kufikia mataifa jirani na hata mpaka wa Israel, kulingana na umbali wa kila aina ya kombora

Silaha muhimu zaidi za Iran ni makombora ya balistiki, ambayo yanaweza kufika kwenye urefu mkubwa wa anga, na yanaweza kufika eneo lengwa kwa njia ya mviringo.

Kulingana na shirika la Foundation for Defense of Democracies, Tehran inayaona makombora yake ya balistiki kama silaha yake yenye nguvu zaidi ya kuleta uharibifu, na ni nguzo muhimu katika ulinzi wake wa anga.

Vikwazo vya kimataifa vinaizuia Iran kununua silaha katika masoko ya kimataifa na hii inahatarisha jeshi lake la anga.

Makombora ya kirusi na ya hypersonic hupaa kwa urefu mdogo wa anga na yanahitaji msaada wa injini za nguvu ya anga (jet au propela) kufikia maeneo lengwa.

Je, mkakati wa Iran wa kutumia makombora umebadilika vipi?

.

CHANZO CHA PICHA, REUTERS

Iran kwa sasa inarusha makombora yake ikilenga Israel na pia mataifa ya Ghuba. Hii ni tofauti na vita vya awali. Awali, Tehran ilikuwa inalenga kundi moja tu, kwenye kambi ya Al-Udeid ya Qatar.

Kulingana na ripoti ya Critical Threats Project, ambayo ipo chini ya kitengo cha utafiti wa sera za Marekani, Iran ilirusha makombora 36 dhidi ya Israeli katika siku nne za mwanzo za vita hivyo.

Idadi kubwa zaidi ya mashambulizi ilirekodiwa siku ya kwanza, ambapo makombora 20 yalirushwa, na wastani wa makombora 2 hadi 3 kwa kila mlipuko.

Mwelekeo huu ulibadilika siku ya pili. Idadi ya mfululizo wa mashambulizi ya kila siku ilipungua hadi mara nne tu siku ya pili, na sita siku ya tatu na ya nne. Wakati huo huo, wastani wa makombora yaliyorushwa na Israel katika kila mlipuko yaliongezeka hadi kati ya 9 na 30 siku ya pili.

Kulingana na Institute for National Security Studies, inayohusiana na Chuo Kikuu cha Tel Aviv, Iran ilirusha makombora 128 dhidi ya Israel kuanzia mwanzo wa vita hadi taehe 4 Machi.

Kulingana na maafisa wa Israeli, Waisraeli 10 waliuawa katika mashambulizi haya kufikia siku ya Alhamisi, lakini hakuna mwanajeshi aliyejeruhiwa.

Iran haijatangaza idadi kamili ya makombora iliyorusha, lakini kwa mujibu wa Kikosi cha Revolutionary Guards ifikiapo tarehe 4 mwezi Machi, siku ya tano ya vita, milipuko 17 ya makombora ilikuwa imerushwa dhidi ya kambi za Marekani katika mataifa ya Ghuba na Israel.

Kulingana na makadirio ya Israeli, Iran imepoteza takriban nusu ya maeneo yake ya kurusha makombora katika vita vya sasa na vya awali.

Kulingana na Nicholas Carl, mkurugenzi msaidizi wa Critical Threats Project, hili limepunguza uratibu kati ya vitengo vya makombora na kuifanya iwe rahisi zaidi kuyazuia.

Carl aliambia BBC kwamba Marekani na Israel zinalenga sana kikosi kinachorusha makombora.

Ingawa ni vigumu kusema maeneo mangapi ya kurusha makombora bado yanafanya kazi nchini Iran, Carl anasema hayako mengi, “idadi ya makombora ambayo Iran inaweza kurusha kwa wakati mmoja imepungua.”

Hata hivyo, kwa maoni yake, hili halipunguzi hatari ya Israel kushambuliwa na makombora ya Iran.

Iran imeongeza mashambulizi dhidi kambi za kijeshi za Marekani zilizoko mataifa ya Ghuba.

Kulingana na takwimu kutoka wizara za ulinzi za UAE, Bahrain, Kuwait, Qatar na Saudi Arabia, BBC imehesabu kwamba Iran ilirusha makombora 551 dhidi ya mataifa ya Ghuba katika siku nne za vita hivyo.

Idadi hii ni kubwa zaidi kuliko vita vya awali, ambapo Iran ilirusha makombora takriban 500 dhidi ya Israel katika kipindi cha siku 12. Nchi hizi zimekosoa mashambulizi ya Iran kwa kusema ni “shambulio lisilokubalika dhidi ya uhuru wao” na zimeeleza kwamba makazi ya kiraia pia yalilengwa.

Watu saba waliuawa katika mashambulizi hayo nchini Bahrain, Kuwait, na UAE, huku mtu mmoja akiuawa kwenye kituo cha mafuta kando ya pwani ya Oman. Vifo pia viliripotiwa Iraq na Syria.

Mataifa ya Ghuba bado hayajachukua hatua yoyote ya kijeshi dhidi ya Iran, bali zimezingatia hatua za kujilinda na shinikizo la kidiplomasia.

Mabadiliko haya yametokea vipi?

.

CHANZO CHA PICHA, FADEL SENNA / AFP VIA GETTY IMAGES

kulingana na Nicholas Carl, uamuzi wa Iran kulenga mataifa ya Ghuba umeipa fursa ya kutumia silaha ambazo hazikutumika katika migogoro ya awali.

Anasema kwamba mwezi Juni mwaka uliopita, “Iran ilikuwa inatumia tu silaha zinazoweza kufikia Israel. Sasa inaweza kutumia makombora ya muda mfupi, ikimaanisha kwamba mifumo yote ambayo haikuweza kutumika mwaka uliopita sasa inatumika.”

Iran pia inaendelea kutumia ndege zisizo na rubani aina ya ‘Shahed’, jambo linalomaanisha bado ina mifumo kadhaa hai ambayo wanaweza kutumia.

Kulingana na Jenerali wa Marekani Dean Cain, mashambulizi ya makombora ya balisitiki ya Iran yamepungua kwa 86% ukilinganisha na siku ya kwanza ya vita.

Utegemezi mkubwa wa ndege zisizo na rubani

Kulingana na uchambuzi wa BBC, mashambulizi ya Iran dhidi ya mataifa ya Ghuba yamehusisha ndege zisizo na rubani zaidi kuliko makombora. Kufikia tarehe 4 Machi, ndege 1,493 na makombora 551 tayari yalikuwa yamerushwa dhidi ya mataifa ya Ghuba. Kiasi hiki kimezidi ndege 1,100 ambazo Iran ilirusha dhidi ya Israel wakati wa vita vya siku kumi na mbili.

Kulingana na Carl, mkakati wa Iran huenda ni kujaribu kushinikiza mataifa ya Ghuba kulegeza kamba ili waweze kuongeza shinikizo dhidi ya Washington na Tel Aviv.

Kulingana na Jenerali wa Marekani Dean Kane, mashambulizi ya ndege zisizo na rubani ya Iran yamepungua kwa 73% ukilinganisha na siku ya kwanza ya vita.

Inawezekana kwamba Iran inajaribu kudumisha hifadhi yake kwa sababu inazidi kuwa vigumu kuzalisha silaha hizo kwa haraka.

.

CHANZO CHA PICHA, REUTERS

Iran inaweza kuendelea kurusha makombora kwa muda gani?

Israel inakadiria kuwa Iran ilikuwa na makombora ya balisitiki takriban 2,500 kabla ya vita. Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Marco Rubio amesema kuwa Iran inazalisha makombora takriban 100 kila mwezi. Makadirio haya hayawezi kuthibitishwa kikamilifu.

Kulingana na Carl, hifadhi ya Iran mwishowe itapungua hadi viwango hatarishi, lakini ni vigumu kusema lini hili litatokea.

Kwa maoni yake, Iran itaendelea na mkakati wake wa sasa, ambayo ni mashambulizi makubwa ya makombora yataendelea katika eneo hilo.

“Iran wanajua kwamba makombora yao mengi yatazuiliwa na mifumo ya ulinzi”

Rais wa Marekani Donald Trump anadai kuwa Marekani ina “silaha zisizo na kikomo,” huku wizara ya ulinzi ya Iran ikisema ina uwezo wa “kupigana kwa muda mrefu zaidi kuliko Marekani inavyotarajia.”

Mashambulizi ya Marekani na Israel

Marekani na Israel zinaendelea kutumia nguvu zao za anga kuishambulia Iran. Marekani pia imekuwa ikirusha makombora kutoka ardhini na baharini.

Kulingana na CENTCOM, katika siku nne za kwanza za vita, Marekani ilifanya mashambulizi 2,000, ikitumia mabomu zaidi ya 2,000.

Israel ilifanya mashambulizi ya anga 600 hadi tarehe 4 mwezi Machi. Katika kipindi hiki, jeshi la anga la Israel liliangusha jumla ya mabomu 5,000.

Kulingana na Hilal-e Ahmar raia 1,045 waliuawa katika mashambulizi haya, wakiwemo watoto 175 na wafanyakazi wa shule waliouwawa katika shambulio la makombora kwenye shule ya msingi huko Minab siku ya kwanza ya vita.

Haijulikani kama idadi hii inajumuisha wanajeshi wa Revolutionary Guards.

Ufitinema Aime Gerard

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *