Mataifa yenye nguvu kubwa za kijeshi duniani
Nguvu ya kijeshi ya taifa fulani ni zaidi ya idadi ya wanajeshi wanaowamiliki.
Nguvu ya kijeshi inahusisha, bajeti za ulinzi, vifaa vya kisasa, na uwezo wa kimkakati hii ni kulingana na mtandao wa habari wa The NationOnline nchini Nigeria.
Kupitia matumizi ya bajeti ya ulinzi, mifumo ya kuzuia silaha za nyuklia, na silaha za kisasa, mataifa yenye nguvu kubwa za kijeshi duniani ni Marekani, Urusi na China.
Miundo yao ya kijeshi inajumuisha ulinzi wa anga, meli za kisasa za kivita, kambi za kijeshi katika mataifa ya kigeni na uwezo wa kujilinda kwenye mtandao.
Kulingana na Global Firepower Index 2026, hizi ndizo nchi 10 zenye nguvu kubwa za kijeshi duniani.
Marekani
CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES
Marekani inaongoza duniani kwa kuwa na idadi kubwa ya wanajeshi, akiba kubwa ya rasilimali za kijeshi, na bajeti kubwa zaidi ya ulinzi.
Kutokana na rasilimali zake Marekani ina teknolojia ya kisasa ya kivita, na uwezo wa hali ya juu wa anga, baharini, na mtandaoni.
Marekani ina wanajeshi wanaohudumu 1,328,000, wanajeshi wa akiba 2,127,000 na bajeti ya ulinzi ya dola bilioni $895.
Urusi
Urusi ina nguvu kubwa za nyuklia, akiba kubwa ya wanajeshi, na mifumo ya kisasa ya magari ya kivita na makombora.
Urusi ina wanajeshi 1,320,000, wanajeshi wa akiba 3,570,000 huku bajeti yao ya ulinzi ikiwa dola billioni $126.
China
CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES
China inaongoza kwa kuwa na jeshi kubwa la kutoa huduma kote duniani, na pia ina uwezo mkubwa wa anga na baharini pamoja na teknolojia ya kisasa.
Idadi ya wanajeshi wanaohudumu nchini China ni 2,035,000, idadi ya wanajeshi wa akiba ni 3,045,000, huku bajeti yao ya ulinzi ikiwa dola billioni $266.85.
India
CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES
India ina mojawapo ya majeshi yenye nguvu zaidi duniani, wakiwa na uwezo wa nyuklia na akiba kubwa ya wanajeshi. India ina ushawishi wa kikanda bara Asia.
India ina wanajeshi wanaohudumu 1,455,550, wanajeshi wa akiba 5,137,000 na bajeti dola billioni $75.
Korea Kusini
Korea Kusini imewekeza katika teknolojia ya kisasa, akiba kubwa ya silaha, na maandalizi makubwa ya ulinzi. Jeshi lake limeundwa kukabiliana na vitisho vya kikanda, hasa kutoka Korea Kaskazini.
Idadi ya wanajeshi wanaohudumu nchini Korea Kusini ni 600,000, wanajeshi wa akiba 3,800,000 na bajeti ya ulinzi ya dolla billioni $50.
Uingereza
Uingereza ina jeshi linalotumia teknolojia ya kisasa lenye uwezo wa kujilinda kutokana na silaha za nyuklia, ina uwezo mkubwa wa baharini na kikosi kikubwa kinachoweza kutumwa kote duniani.
Wanajeshi wake wanaohudumu ni 144,400, wanajeshi wa akiba 215,050 na bajeti ya ulinzi ni dolla billioni $71.5.
Ufaransa
Ufaransa ina jeshi lenye vifaa vya kisasa, uwezo wa nyuklia, ndege za kisasa, na uwezo wa kuingilia kati duniani kote.
Wanajeshi wanaohudumu nchini Ufaransa ni 270,000, wanajeshi wa akiba ni 474,750 huku bajeti ya ulinzi ikiwa dolla billioni $63.7.
Japan
CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES
Vikosi vya kujilinda vya Japan vimejikita katika teknolojia ya kisasa, ulinzi dhidi ya makombora, na usalama wa baharini. Ushirikiano wa kimkakati na washirika wake unaisaidia kuimarisha utulivu wa kikanda.
Idadi yake ya wanajeshi wanaohudumu ni 247,000, wanajeshi wa akiba ni 317,600 huku bajeti ya ulinzi ikiwa dolla billioni $57.
Uturuki
Uturuki ina jeshi kubwa la wanajeshi wanaohudumu na wa akiba, huku ikiwa na uwezo wa uzalishaji wa silaha za ndani ya nchi hiyo, ina uwezo mkubwa wa ndege zisizo na rubani, na ina ushawishi wa kikanda katika Mashariki ya Kati.
Wanajeshi wanaohudumu ni 355,200, wanajeshi wa akiba 890,700 huku bajeti ya ulinzi ikiwa dola billioni $20 .
Italia
Italia ina jeshi la kisasa linalokidhi viwango vya NATO, likiwa na meli za kubeba ndege za kivita, uwezo wa ulinzi wa mtandao, na hushiriki katika operesheni za kimataifa na oparesheni za kulinda amani.
