Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu: Manchester United inamtaka Victor Osimhen
Manchester United inataka kumsajili mshambuliaji wa Nigeria Victor Osimhen, 26, kutoka Napoli, ambayo inatathmini uwezekano wa kumpata mshambuliaji wa Denmark Rasmus Hojlund, 22, kama sehemu ya mkataba huo. (Calciomercato – kwa Kiitaliano)
Manchester City na Manchester United zinamfuatilia kwa karibu winga wa Ureno Francisco Trincao, ingawa Sporting ina matumaini ya kufikia kandarasi mpya na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25. (A Bola – kwa Kireno)
Manchester United ina mpango wa kumnunua kiungo wa Real Sociedad na Uhispania Martin Zubimendi, 26. (GiveMeSport)
Everton inataka kumsajili winga wa Brazil Luis Henrique, 23, kutoka Marseille msimu huu wa joto lakini watakabiliana na ushindani kutoka kwa Newcastle na Nottingham Forest. (Football Insider)
West Ham wana nia ya kumsajili beki wa Genoa wa Mbelgiji Koni de Winter, 22. (Nicolo Schira)
Tottenham na Brighton ni miongoni mwa vilabu kadhaa vinavyowania saini ya beki wa Romania Andrei Ratiu, 26, anayekipiga katika klabu ya Rayo Vallecano. (Mundo Deportivo – kwa Kihispania)
Liverpool inamfuatilia beki wa Denmark Anton Gaaei, 22, na mshambuliaji wa Ubelgiji Mika Godts, 19. (TBR Football)
Tottenham iko tayari kuongeza dau lao ka pauni milioni 8.5 kumsajili mshambuliaji wa Ujerumani Timo Werner msimu huu wa joto baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 kuondoka RB Leipzig kwa mkopo. (Mirror)
Newcastle ikotayari kumuuza mlinda lango wao wa Uingereza Nick Pope, 32, kwa kati ya pauni milioni 10-15 na wana nia ya kumbadilisha na kipa wa Burnley mwenye umri wa miaka 22 James Trafford. (Football Insider)
Barcelona inatazamia kuongeza mkataba wa winga wa Brazil Raphinha, 28. (Mundo Deportivo – kwa Kihispania)
Chelsea bado iko mbioni kumsaka kiungo wa Gremio na Brazil Gabriel Mec, 16. (TBR Football)