Tetesi za soka Ulaya Alhamisi: Arsenal yaangalia uwezekano wa uhamisho wa Rodrygo

Tetesi za soka Ulaya Alhamisi: Arsenal yaangalia uwezekano wa uhamisho wa Rodrygo

Arsenal inataka kumnunua mshambuliaji wa Brazil Rodrygo, 24, ambaye anaweza kuondoka Real Madrid msimu huu wa joto. (Sky Germany)

Kiungo mshambuliaji wa Bayer Leverkusen Florian Wirtz anatarajiwa kuchagua kati ya kuhamia Bayern Munich na Liverpool ndani ya siku 10 zijazo, huku klabu zote zikiwa na hamu ya kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani, 22. (Kicker – In Germany)

g

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, Luis Diaz

Barcelona wanataka kumsajili winga wa Liverpool mwenye umri wa miaka 28 kutoka Colombia Luis Diaz, ambaye amebakiza miaka miwili kwenye mkataba wake wa Anfield. (ESPN)

Liverpool wanamfuatilia winga wa Lyon na Ubelgiji Malick Fofana mwenye umri wa miaka 20 kama chaguo linalowezekana ikiwa Diaz ataihama klabu hiyo. (Mundo Deportivo – in Spanish).

g

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, Kevin de Bruyne,

Napoli na Chicago Fire wanaongoza katika mbio za kumsajili kiungo wa kati wa Ubelgiji Kevin de Bruyne, 33, ambaye ataondoka Manchester City kama mchezaji huru msimu huu wa joto. (Sport)

Kiungo wa kati wa Manchester City James McAtee analengwa na Bayer Leverkusen, huku Mwingereza huyo mwenye umri wa miaka 22 pia akifuatiliwa na vilabu kadhaa vya Primia Ligi. (Sky Germany)

g

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, Enzo Fernandez

Chelsea wamedhamiria kumshikilia kiungo wa kati wa Argentina Enzo Fernandez, licha ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 kuwa kwenye orodha fupi ya Real Madrid ya wachezaji wanaoweza kuwindwa msimu huu. (Guardian)

Liverpool wamempa beki wao wa kati wa Uhispania Wellity Lucky, 19, mkataba mpya wa miaka minne. (Fabrizio Romano),

g

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, Moise Kean

Rais wa Fiorentina Rocco Commisso anatazamiwa kukutana na mshambuliaji wa Italia Moise Kean kujaribu kumshawishi mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 kusalia huku kukiwa na nia ya vilabu kadhaa. (Football Italia)

Viktor Gyokeres amewaambia wachezaji wenzake wa Sporting kuwa hana uhakika atacheza wapi mwaka ujao, huku mshambuliaji huyo wa Sweden mwenye umri wa miaka 26 akihusishwa na Arsenal na Manchester United. (Canal 11, via Star).

Ufitinema Aime Gerard

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *